Prof. Janabi achaguliwa kuwa Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambaye pia ni Mshauri wa Rais wa Tanzania Masuala ya Afya na Tiba Profesa Mohamed Yakub Janabi amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika katika uchaguzi uliofanyika leo Mei 18,2025 Geneva.