Diamond apewa elimu Taratibu za kufuata Viwanja vya ndege

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bw. Abdul Mombokaleo, leo amekutana na Msanii maarufu Bw. Naseeb Abdul Juma alimaarufu Diamond Platnumz kwa ajili ya mazungumzo yaliyolenga taratibu za kufuata katika viwanja vya ndege wakati wa safari za ndani na nje ya nchi katika Ofisi za makao Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalilenga pia kumuwezesha msanii huyo akiwa kama kioo cha jamii kutoa elimu kwa wasanii wengine juu ya miongozo, taratibu na sheria za kufuata katika viwanja vya ndege.


Msanii huyo amemshukuru Mkurugenzi Mkuu na Menejimenti ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa Elimu hiyo na kuahidi kuwa balozi mzuri kwa wasanii wengine ili kuepusha taswira mbaya kwa Taasisi na wasanii pia.

Katika mazungumzo hayo Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Bi. Bertha Bankwa alimpongeza Diamond Platnumz kwa kuchukua hatua za kupata elimu ya matumizi sahihi ya Viwanja vya Ndege na kuahidi kuendelea kutoa elimu mara kwa mara ili kuboresha huduma katika Viwanja vya Ndege.