Silaha Mbili pistol aina ya Retay C91C yenye namba R1YGCMOY01-24004425 CAL 9MM ikiwa na risasi 150 kwenye kasha zake tatu ndani ya begi lake jeusi pamoja katika maegesho ya magari majengo Tunduma likiwa limetelekezwa huku ikibainika kuingia nchini sivyo kihalali na aina ya pili ni CZ92 BROWNING yenye namba A 428007 ,caliber 6.35mm ikiwa na risasi sita yenye rangi ya gold na weusi ambayo ilikamatwa Mei 14,2025 maeneo ya black Market Tunduma Wilayani Momba.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe Kamshina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP)Augustino Senga amethibitisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema Jeshi hilo linaendelea na msako wa kumtafuta mtu ama watu waliohusika na tukio hilo.
Aidha Kamanda Senga amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na kufichua wahalifu katika maeneo yao.
Leave a Reply