Bunge la Seneti la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) limeidhinisha hatua ya kumuondolea kinga ya kisheria aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila, hatua inayomfungulia njia ya kufunguliwa mashitaka mbalimbali ikiwemo uhaini na uhalifu wa kivita.
Katika kikao cha Seneti kilichofanyika Alhamisi, Mei 22, maseneta 88 walipiga kura ya kumuondolea kinga, watano wakapinga, huku kura tatu zikibatilishwa. Kabila hakuhudhuria kikao hicho wala kujieleza mbele ya bunge hilo, huku taarifa zikieleza kwamba aliondoka nchini tangu mwaka 2023.
Kabila, ambaye ni seneta wa maisha kwa mujibu wa katiba ya DRC tangu kuondoka madarakani mwaka 2019, anatuhumiwa kwa uhaini, uhalifu wa kivita, na kuunga mkono kundi la waasi la M23 ambalo liliteka miji mikubwa Mashariki mwa Congo mapema mwaka huu.
Leave a Reply