Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu, amechaguliwa kuwa mmoja wa Makamu Wenyeviti wa Muungano wa Vyama vya Kidemokrasia Duniani (International Democrat Union – IDU) katika uchaguzi uliofanyika jijini Brussels, Ubelgiji.
Uchaguzi huo ulikuwa sehemu ya hitimisho la mfululizo wa mikutano ya IDU ambapo pia Waziri Mkuu Mstaafu wa 22 wa Canada, Stephen J. Harper, alichaguliwa tena kuendelea kuwa Mwenyekiti wa umoja huo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Katika uchaguzi huo, CHADEMA iliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Democracy Union of Africa (DUA) Kanda ya Afrika Mashariki, Mheshimiwa Deogratias Munishi. Wajumbe wa mkutano huo walimchagua Lissu kwa kauli moja kutokana na msimamo wake thabiti katika kupigania haki za binadamu, demokrasia na utawala bora nchini Tanzania.
Leave a Reply