Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka
watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na uzalendo,
wakizingatia viapo vyao kwa vitendo,
Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo alipokuwa akiwaapisha viongozi aliowateua hivi
karibuni katika hafla iliyofanyika Ikulu, ambayo pia ilihusisha kiapo cha maadili kwa
viongozi waliokwishateuliwa siku za nyuma
Viongozi walioapishwa ni Prof. Tumaini Joseph Nagu aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEM) anayeshughulikia
masuala ya afya; Dkt. Blandina Buganzi Kilama aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mtendaji
wa Tume ya Mipango anayeshughulikia biashara na ubunifu; na Jaji Mstaafu John Samweli
Mgetta aliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili,
Rais Dkt. Samia amewataka viongozi hao kushirikiana kikamilifu katika kazi na watumishi
wa ofisi wanazokwenda, kuheshimu maadili ya utumishi wa umma na kuwa mfano wa
uongozi bora kwa ajili ya maendeleo ya Taifa
Kadhalika, Rais Dkt. Samia amewaagiza viongozi wa Tume ya Mipango kushirikiana katika
uratibu wa miradi mikubwa ya kitaifa na kuhakikisha kuwa inafungamana na malengo ya
kitaifa;
Kwa upande wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Rais Dkt. Samia amelielekeza
Shirika hilo kuendeleza vyanzo vidogovidogo vya uzalishaji umeme nchini, kusimamia
usambazaji wa umeme wa uhakika unaozalishwa pamoja na kutathmini uzalishaji umeme
kwa vyanzo vya nishati jadid
Leave a Reply