SIMIYU – Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewataka wafugaji nchini kuhakikisha wanazingatia sheria ili kudhibiti migogoro ya kuingiza mifugo hifadhini pamoja na ile ya wakulima, ambayo imesababisha kuwepo kwa kesi nyingi mahakamani.
Balozi Dkt. Nchimbi aliyasema hayo leo Juni 15, 2025, wakati wa Kongamano la Wafugaji Kitaifa lililofanyika katika viwanja vya Nanenane, Nyakabindi, Halmashauri ya Mji Bariadi, Mkoani Simiyu. Kongamano hilo linafunguliwa na Balozi Dkt. Nchimbi na litahitimishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Naye Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema Wizara inatekeleza majukumu yake na imeweka kipaumbele cha kushirikiana na wadau wanaozalisha mazao ya mifugo kwa lengo la kuhakikisha sekta ya mifugo inakua.
Aidha, Waziri Dkt. Kijaji amewataka wafugaji kuona na kutambua umuhimu wa Chanjo ya Kitaifa pamoja na Utambuzi wa Mifugo, kampeni ambayo inatarajiwa kuzinduliwa na Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ifikapo Juni 16, 2025, katika eneo la Nyakabindi, Halmashauri ya Mji Bariadi.
Leave a Reply