Leo Jumapili, Juni 15, 2025, waumini wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church, maarufu kama Kanisa la Ufufuo na Uzima, walijitokeza kufanya ibada katika eneo la Ubungo. Baada ya kushusha maombi yao, waliamua kuingia barabarani wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali, zikionyesha kupinga kuzuiwa kuabudu ndani ya kanisa hilo.
Kufuatia hatua hiyo ya waumini kuingia barabarani, Jeshi la Polisi limelazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya.
Leave a Reply