Kesi ya uhaini dhidi ya lissu yapigwa kalenda, wakili jebra azungumza kwa uchungu

Wakili Jebra Kambole ni miongoni mwa Mawakili wapatao 30 wanaomtetea Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu katika kesi ya Uhaini dhidi ya Jamhuri, ambapo amezungumza kuhusu uamuzi wa Lissu kutaka kujitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo pamoja na sababu alizitoa, ikiwemo madai ya mawakili wake hao kunyimwa fursa ya kukutana na kuzungumza naye faragha.

Jebra amesema kwakua Tundu Lissu ni Wakili mzoefu na aliwahi kuwa hadi Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), wana imani ya kuwa uwezo wa kusimama mwenyewe kwenye kesi hiyo anao.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Franco Kiswaga ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 1, 2025 ambapo imeelezwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali atatoa tarehe rasmi ya kesi hiyo kwenda Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa.