Jay-Z Adaiwa Atatumbuiza Superbowl 2026.

Kwa Mujibu Wa Ripoti Mbalimbali Nchini Marekani Ni Kwamba Huenda Rapa Jay-Z akatumbuiza Kwenye Fainali Za Superbowl (Halftime Show) Mwakani 2026.

Taarifa Hii Inakuja Baada Ya Kutumbuiza Kwa Mara Ya Kwanza Baada Ya Miaka 7 Kwenye Ziara Ya Beyonce ‘Cowboy Carter’ Juzi Jijini Paris, Ufaransa.

Jay-Z Ambaye Ni Mtaalam Na Mpanga Mikakati Wa Muziki Wa NFL Kupitia Ushirikiano Wa Kampuni Yake ‘Roc Nation’ Bado Hajaibuka Na Kuthibitisha Taarifa Hizi.

Je, Ikiwa Kweli Jayz Atatumbuiza Superbowl Unatamani Atumbuiza Wimbo Gani ⁉️