Trey Sonhz Alivyotaka Kupigana Baada Ya Kuletewa Dharau.

Kwa mujibu wa video na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Trey Songz alionekana akiongea kwa hasira huku akitoa maneno ya vitisho ya wazi, akieleza nia ya kumpiga mwanaume huyo kutokana na kile alichokitaja kama “kuoneshwa dharau.”

Hata hivyo, hadi sasa, jina na utambulisho wa mwanaume aliyelengwa na vitisho hivyo haujafahamika rasmi. Mashabiki pamoja na watu mbalimbali mitandaoni wanaendelea kufuatilia kwa karibu wakisubiri taarifa zaidi kuhusu kile kilichojiri, chanzo halisi cha mzozo huo, pamoja na msimamo wa Trey Songz au timu yake ya usimamizi.

Tukio hili limeibua hisia mseto mitandaoni, baadhi wakimkosoa msanii huyo kwa kuonesha hasira kupita kiasi, huku wengine wakionyesha uelewa na kutaka kusikia upande wake wa hadithi.

Trey Songz, ambaye kwa muda mrefu amekuwa gumzo si tu kwa vipaji vyake vya muziki bali pia kwa matukio mbalimbali ya utata nje ya jukwaa, sasa anakabiliwa na presha ya kutoa maelezo au tamko rasmi juu ya tukio hilo linaloendelea kuzua mjadala.