Ahukumiwa Jela miaka 60 kwa kubaka wanafunzi wawili

Mahakama ya Wilaya ya Mkinga, mkoani Tanga, Julai 17, 2025 imemhukumu Sadi  Mtangi, mkazi wa Maramba, kifungo cha miaka 60 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili ya kubaka wanafunzi wawili wa kike wenye umri wa miaka 13 na 9.

Awali, ilielezwa mahakamani kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kuanzia tarehe 11 Agosti 2024 dhidi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Maramba na Shule ya Msingi Mapatano, wote wakazi wa Maramba.

Akisoma hukumu hiyo, Mheshimiwa Hakimu Deda alisema kuwa mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kumhukumu mtuhumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kila kosa, adhabu itakayotekelezwa mfululizo.