Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeyakataa maombi ya Tundu Lissu kupitia shauri la marejeo la kupinga matumizi ya mashahidi wa siri kama ilivyoombwa na Jamhuri katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Akizungumza nje ya mahakama, baada ya kusikilizwa kwa shauri hilo ambalo uamuzi wake umetolewa Agosti 12, 2025 mbele ya Jaji Elizabeth Mkwizu, Wakili wa Lissu Dkt.
Rugemeleza Nshala amesema hawajaridhishwa na uamuzi huo wakidai kuwa suala hilo linapoka haki ya mshtakiwa, hivyo wataketi na mteja wao kwa ajili ya muafaka wa hatua stahiki za kuchukua.
Leave a Reply