Kesi Ya Lissu Yapigwa tena Kalenda hadi Agosti 18

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imeahirisha kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu hadi Agosti 18, 2025, ili kutoa amri kuhusu ombi na mapingamizi ya urushaji wa moja kwa moja wa mwenendo wa shauri hilo.

Uamuzi ni kufuata upande wa Jamhuri kuomba kesi hiyo isirushwe mubashara kwa lengo Ia kulinda utambulisho wa mashahidi raia, ombi ambalo limepingwa na upande wa utetezi ukidai kuwa haina mashiko.

Akiahirisha kesi hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Franco Kiswaga, amesema mawasilisho ya pande zote mbili hayatohitaji muda wa kutosha kwa maandalizi ya hukumu, bali yatahitaji amri ndogo zinazohusu utaratibu wa shauri, na kuwa kwa mujibu wa maagizo ya Mahakama Kuu kuhusu ulinzi wa mashahidi, wanaopaswa kulindwa ni mashahidi raia pekee.