Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza ratiba ya vikao vyake muhimu vya kitaifa vitakavyofanyika jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa NEC, itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA. Amos Makalla leo Agosti 17, 2025 Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitafanyika tarehe 21 Agosti 2025, kikifuatiwa na Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa kitakachofanyika tarehe 23 Agosti 2025.
Ajenda ya vikao hivyo itakuwa ni uteuzi wa; Wagombea Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Viti Maalum, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum.
CCM yatangaza ratiba ya vikao vya uteuzi wa wagombea Ubunge

Leave a Reply