Simba 🦁 @diamondplatnumz Ameandika Ujumbe Mwingine Kwa @mbosso_ Kuhusu Namna Walivyoshauriana Katika Uandaaji Wa Ep Yake Ya ‘Khan’ Lakini Pia Wakati Ambao Mbosso Alikuwa Hapewi Thamani Na Kuonekana Hajui Muziki.
“Umekamilisha epumekuja home tunashauriana
namna ya promotion, logo ya khan music, tarehe ya kurelease ep, maviewers ya mpaka media coverage na kila kitu ili nawe ep yako ikafanye vizuri, leo ukaseme”
“chana na mabongo fleva ya kina mbagala, ukimuona, zuwena, sikomi yenye milioni 70 youtube, makolabo from yope, love you die, tetema, enjoy etc? yani nakuonea wivu yani nilikuwa na sababu ipi ya kuweka mawazo yangu kwenye ep ikiwa ushatoka wasafi sasa, au nakuonea gere yani kwa hit hit ipi labda unayofikiri wewe
ilohit kuliko komasava, wah, inama, baba lao, number one, jeje, african beauty etc…!?”
“yani nikuonee wivu kwa kipi labda ambacho mie nakitamani kwako?? muziki ni safari ndefu mdogo angu usikubali kupumbazwa na wajinga ukagombana na watu wenye upendo wa kweli kwako na kukupambania pindi wengi hawakuthamini… si walikua wanakukataa na kusema huna uwezo kipaji anacho aslay na daftari kaondoka nalo, leo umekua wa maana sana eeh? jifunze kuijua dunia na watu wake! jifunze kujua wanafiki na watu real kwenye maisha!” – Diamond Platnumz

Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.