Miili miwili yaopolewa Mgodini Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amethibitisha kutolewa kwa miili ya watu wengine wawili waliokuwa wamefukiwa kwenye ajali ya Mgodi wa Kikundi cha Wachapakazi katika machimbo ya Nyandolwa wilayani Shinyanga na hivyo kupelekea idadi ya waliopolewa kutoka ardhini mpaka sasa kufikia kumi.

Wawili hao waliopolewa walikuwa kwenye duara namba 20 C ambao ni Japhet Masanja (30) mkazi wa Lunguya wilayani Kahama, na Chembanya Makenzi (25) mkazi wa Nyandolwa wilayani Shinyanga.ambapo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni mhita amethibitisha kuhusu ongezeko la miili hiyo miwili

Akielezea hali ya uokoaji RC Mboni amesema, zoezi la uokoaji linakwenda vizuri na timu za waokoaji zimefanikiwa kutengeneza njia za kuwapata watu ambao wamesalia kuokolewa, huku akianisha kuwa jumla ya watu kumi na tano wamesalia aridhini

“Tumetoa Miili ya watu wengine wawili,jumla kuu mpaka sasa waliotolewa ni Watu kumi , na waliosalia aridhini ni watu kumi na tano ”amesema RC Mboni.

Agosti 11 mwaka huu, watu ishirini na tano walifukiwa na Mgodi wa Kikundi cha Wachapakazi katika Machimbo ya Nyandolwa wilayani Shinyanga,ampapo watu kumi wameopolewa na watatu miongoni mwao wakiwa hai na saba wakifariki dunia kutokana na janga hilo.