Dkt. Samia aongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM

DODOMA – Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 21, 2025 ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika jijini Dodoma.

Kikao hicho kilikuwa na ajenda kuu ya kufanya uteuzi wa wagombea mbalimbali wa chama hicho. Uteuzi huo unajumuisha Wagombea Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Viti Maalum, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum.