Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya DCEA imesema mwanamuzi wa kizazi kipya Chid Benz, akirudi kwenye matumizi ya dawa za kulevya atachukuliwa hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.
Kauli hiyo imetolewa na kamishina jenerali wa DCEA Aretas Lyimo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika tukio la lumkabidhi Chid Benz kwa jamii yake mara baada ya kumaliza matibabu ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.
Kamishina Lyimo ameongeza kuwa serikali imetumia gharama kubwa katika matibabu ya watu mbalimbali wanaotumia dawa zake kulevya na mpaka sasa zaidi ya watu milioni moja wamepata matibabu bure kupitia serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Leave a Reply