Makalla ateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, CPA. Amos Gabriel Makalla ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kabla ya uteuzi huu, CPA. Makalla alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi, na anachukua nafasi ya Bw. Kenan Laban Kihongosi ambaye ameteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi.

Uapisho wa Mkuu wa Mkoa Mteule utafanyika tarehe 26 Agosti, 2025