Baba Levo Achukua Fomu Kugombea Ubunge Kigoma Mjini

Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Clayton Chipando maarufu kama @OfficialBabaLevo amechukua fomu kwenye ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jimbo la Kigoma Mjini kwa ajili ya kugombea Ubunge.

Baba Levo amechukua fomu hiyo leo Agosti 26, 2025 akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa CCM jimbo la Kigoma Mjini.