Tembo watatu wazua kizaazaa Manispaa ya Singida

Wanyamapori Watatu Aina ya Tembo Wamevamia Makazi ya Wananchi wa Kata ya Unyianga Mkoani Singida na Kuzua Hofu kwa Wananchi huku Mamlaka za Serikali TAWA,TAWIRI na Askari wakifanikiwa kuwadhibiti Wanyama hao.

Wakizungumza mara baada ya kudhibitiwa Wanyama Hao wananchi wa Kata ya unyianga wameeleza namna walivyoshtushiwa na Tukio Hilo huku wakiiomba Serikali iwadhibiti Wanyama hao wasiwe wanafika katika Makazi ya Watu.

Viongozi waliojitokeza katika Tukio hilo wamesema Hakuna Vifo wala Uharibifu wa Mali za wananchi ambao umeriporitiwa kufuatia Tukio hilo.

View this post on Instagram

A post shared by Wasafi FM (@wasafifm)