Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma, leo imesikiliza shauri la kupinga kuzuiliwa kurudisha fomu ya uteuzi kwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo Ndugu Luhaga Joelson Mpina.
Shauri hilo limesikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu. Baada ya usikilizwaji, Mahakama imejipa muda wa siku tatu kwa ajili ya kutafakari hoja zilizowasilishwa na pande zote.
Kwa mujibu wa maelekezo ya Mahakama, hukumu ya kesi hiyo inatarajiwa kutolewa tarehe 11 Septemba 2025.
Leave a Reply