Msanii Kutoka Marekani @d4vddd (20) Amepata Streams Nyingi Zaidi Kwa Siku Katika Mtandao Wa Spotify tangu aanze Muziki. D4vd anatajwa kupata wasikilizaji Milioni 12.1 Siku ya jumapili Tu.
Hata hivyo, mafanikio haya yanakuja katikati ya sakata linalomkabili baada ya polisi kuanzisha uchunguzi kufuatia kupatikana kwa mwili wa Binti mwenye umri wa miaka 15, aitwaye Celeste, ndani ya gari lake aina ya Tesla.
Kumbuka Wiki iliyopita, ripoti zilibainisha kuwa marehemu alikuwa na tattoo inayofanana na ya D4vd, huku picha, video na hata mashairi ya nyimbo zake zikionekana kumhusu Celeste, jambo lililozua mjadala mkubwa mitandaoni.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.