Jeshi la Polisi Tanzania limeeleza kuwa linaendelea kumsubiri, Humphrey Polepole, kufika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ili kutoa maelezo kuhusu tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Jeshi la Polisi, Polepole alitumiwa barua ya wito kwa mujibu wa sheria, lakini hadi sasa hajajitokeza kama alivyotakiwa kufanya.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi limesema limeona taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa baadhi ya ndugu wa Polepole wakidai kuwa ametekwa. Polisi wamesema wameanza kufanyia kazi taarifa hizo ili kubaini ukweli wake.
#WasafiDigital
Polisi waanza Kufanyia kazi Taarifa za Polepole kufaiwa Kutekwa

Leave a Reply