Trump Adai Hana Uhakika Kama Ataenda Mbinguni.

Rais Wa Marekani Trump Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Ndani Ya Air Force One Amesema Kwamba Haamini Kama Kuna Jambo Lolote Linaweza Kumpeleka Mbinguni.

“Sidhani kama kuna kitu chochote kitakachonipeleka mbinguni. Kweli, sidhani. Huenda mimi si mtu wa kwenda mbinguni. Labda niko mbinguni sasa hivi, tunaposafiri kwa ndege ya Air Force One. Sina uhakika kama nitaweza kwenda mbinguni, lakini nimefanya maisha ya watu wengi kuwa bora zaidi.

Amesema Trump Baada Ya Kauli Yake Wiki Kadhaa Zilizopita kudai Kutaka Kuimaliza Vita Ya Ukraine Kwani Itamsaidia kwenda mbinguni.