Rapa Playboi Carti Akamatwa Kwa Kumpiga Mpenzi Wake.

Rapa Playboi Carti ameripotiwa kukabiliwa na kesi ya shambulio dogo huko Utah baada ya kutokea ugomvi kati yake, mpenzi wake, na dereva tarehe 2 Oktoba wakati wa Antagonist Tour mjini Park City.

Dereva, Carl Reynolds, anadai ugomvi ulianza baada ya Carti na mpenzi wake kubishana kuhusu masuala ya kimapenzi.

Reynolds anasema Carti alitishia kuwapiga wote wawili kisha akampiga mpenzi wake kifuani na baadaye kumrushia ngumi usoni, jambo lililosababisha uvimbe na maumivu ya shingo kabla ya walinzi kuingilia kati.