SIMBA 🦁 @diamondplatnumz ametangaza rasmi kuleta msimu wa pili wa tamasha lake kubwa la “Diamonds Are Forever”, ambalo linatarajiwa kufanyika mwaka huu kama ishara ya shukrani na upendo kwa industry nzima ya muziki wa Tanzania, na hasa kwa mashabiki waliomuunga mkono tangu mwanzo wa safari yake ya muziki.
Tamasha hili ni mwendelezo wa lile la kwanza lililofanyika mwaka 2012 Mlimani City, ambalo liliweka historia kubwa katika tasnia ya muziki wa Tanzania.

Tamasha la “Diamonds Are Forever” lilikuwa la kwanza kuonyesha uthubutu wa kutengeneza tamasha la Bongo Fleva lililofungua milango katika sekta ya matamasha ya muziki wa Bongo Fleva kwa kupewa thamani kubwa inayostahili. Kwa mara ya kwanza, watu waliweza kuhudhuria kwa kulipa viingilio ambavyo hapo awali haikuwahi kufikiriwa kuwa ingewezekana, Kwani watu walilipa viingilio vya TSh 50,000, 100,000, na hata zaidi.

Tamasha hili lilibadilisha kwa ujumla taswira ya thamani ya muziki wa Bongo Fleva, na kufanya sanaa ya muziki itambulike kama biashara rasmi na kubwa inayoweza kuwa mkombozi hasa kwa vijana wengi wa Kitanzania.

Aidha, tamasha la “Diamonds Are Forever” lilikuwa ni sehemu ya mwanamuziki Diamond Platnumz kuwashukuru na kusherehekea kwa pamoja na mashabiki zake.
Kwa sasa, mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona ni kwa namna gani msimu huu mpya wa “Diamonds Are Forever” utazidi kuvunja rekodi na kuendeleza historia ya ukuaji wa sekta ya matamasha ya muziki nchini, pamoja na kuendeleza sanaa ya muziki kwa ujumla.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.