Mapacha waliomuua Mama yao wahukumiwa kunyongwa hadi Kufa

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kusini, Mtwara imewahukumu kunyongwa hadi kufa mapacha wawili Daniel Stephen Seif(Kurwa) (24) mkulima, mkazi wa Kijiji cha mraushi A” Wilaya ya Masasi na Daniford Stephen Seif (24) (Doto) mkulima Mkazi wa Kijiji cha Mraushi A” Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara baada ya kupatikana na hatia ya mauaji kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16, kifungu cha 196 na 197 marejeo ya Mwaka 2022.

Watiwahatiani wote kwa pamoja walitenda kosa hilo tarehe 15.12.2024 Katika Kijiji cha Mraushi “A” kwa kumpiga mama yao mzazi katika paji la uso aliyefahamika Kwa jina la Upendo Methew (42) mkazi wa Kijiji cha Mraushi A” kwakutumia Jembe na mwichi kumsababishia majeraha yaliyopelekea kifo chake.

Watiwahatiani wote wawili walikiri kutekeleza mauaji hayo ya kikatili baada ya kumtuhumu mama yao kuwa anawaroga.

Hukumu hiyo imetolewa Septemba 11, 2025 na Mahakamu Kuu Kanda ya Kusini Mtwara mbele ya Mhe.Jaji wa Mahakama Kuu Martha Mpaze na Mawakili wasomi Justus Revocatus Zegge na Dais Makakala.

#WasafiDigital