CCM yampitisha Asha kumrithi Abbas Mwinyi Kinyang’anyiro cha Ubunge Fuoni

Chama cha Mapinduzi CCM kupitia kikao chake cha Kamati Kuu Maalum ya Halmashauri kuu imempitisha ndugu Asha Hussein Salehe kupepurusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Ubunge Jimbo la Fuoni Zanzibar

Kupitia taarifa hiyo ya chama cha Mapinduzi CCM imeeleza kuwa Asha Hussein ndie atakaye peperusha bendera ya CCM katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Fuoni Zanzibar kufuatia kufariki kwa aliyekua mgombea Mteule wa nafasi hiyo kupitia CCM Marhem Abbas Mwinyi September 25, 2025

Kwa mujibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania INEC ilitangaza kuwa uchaguzi huo wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Fuoni utafanyika Disemba 30, 2025