The Weeknd Atoa Msaada Wa Dola 350K Jamaica.

Mwanamuziki Kutoka Nchini Canada ‘The Weeknd’ Ameripotiwa kutoa msaada wa $350,000 kupitia XO Humanitarian Fund kusaidia Jamaica baada ya Kimbunga Melissa kusababisha uharibifu mkubwa nchini humo.

Msaada huo, uliotolewa kupitia Mpango wa Chakula wa Dunia wa Umoja wa Mataifa (WFP), utaweza kusaidia kutoa chakula na vifaa vya dharura kwa Wajamaica hadi 200,000 walioathirika na kimbunga hicho. ( hotfreestyle)