
Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi, leo tarehe 22 Januari, 2026 amefungua rasmi Kikao cha 55 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kinachofanyika mkoani Dodoma.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Waziri Ndejembi amemshukuru Mhe. Rais Dkt Samia kwa kuboresha maslahi na stahiki za wafanyakazi wa TANESCO, huku akisisitiza usimamizi madhubuti wa masuala ya haki za wafanyakazi na kuimarisha ushirikiano mahali pa kazi, pamoja na kuendeleza utoaji wa elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu huduma ya umeme.

“Natambua mmekutana hapa kujadili kwa kina mambo yanayowahusu wafanyakazi naomba mhakikishe mnazungumza yote na kukubaliana ili kuendelea kuboresha utendaji wa shirika na maslahi ya wafanyakazi”.
Amehimiza pia umuhimu wa kuendelea kuboresha utoaji wa huduma bora na za uhakika za umeme kwa wateja wake nchini.
Akimkaribisha katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la umeme Bw. Lazaro Twange amemshukuru Mhe Waziri kwa kukubali wito wa kuja kufungua kikao hicho na kumuahidi kuwa wataendelea kusimamia haki za wafanyakazi na kuhakikisha wanakuwa na matokeo katika utendaji.

“Kipekee nikushukuru kwa kuitikia wito wa kuja kutufungulia kikao hiki, kama Mwenyekiti wa baraza hili nikuahidi kuwa nitaenda kuyasimamia yote tutakayojadili hapa kwa ajili ya kuleta tija na maendeleo ya Shirika hili na kuongeza ufanisi katika kuhudumia wananchi”, alieleza Twange.
Kikao hicho kimewakutanisha viongozi wa TANESCO, wawakilishi wa Chama cha Wafanyakazi (TUICO), Wakurugenzi wa Kanda, pamoja na wawakilishi wa wafanyakazi kutoka kampuni tanzu na ofisi mbalimbali za mikoa nchini














Leave a Reply