Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi ameitahadharisha jamii ya Watanzania juu ya vipande vya video vinavyotengenezwa na kusambazwa katika mitandao ya kijamii ambavyo huleta taharuki na suala la kushambulia watu binafsi, akiahidi kusimamia utawala wa sheria huku akihoji kila mtu kuwa msemaji katika nchi.
Ametoa kauli hiyo wakati wa Kikao chake cha Kwanza na Menejimenti ya Wizara hiyo,ambacho kimefanyika leo jijini Dodoma akigusia jukumu la amani na utulivu ni la kila mtanzania ambapo Naibu Waziri,Ayoub Mohamed Mahmoud amesema matumaini ya Watanzania kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni makubwa na watumishi wote wa wizara kwa ujumla wake ndio watekelezaji wa majukumu ili matarajio yaweze kufikiwa















Leave a Reply