A$AP Rocky amekataa ofa ya makubaliano ya kukiri kosa Ili Kupunguziwa Adhabu Ya Kifungo Katika shtaka la jinai linalomkabili ambapo anadaiwa kumpiga risasi rafiki yake wa zamani, #ASAPRelli huko Los Angeles 2021. Hii Ni kwa mujibu wa ripoti ya Nancy Dillon wa Rolling Stone. Rocky Anaamini Kuwa Ni Mpango Wa Kumuangushia Jumba Bovu.
Waendesha mashtaka walimpa Rapa huyo Ofa Ya kifungo cha nje cha miaka 3, Huku Wakiahidi Kusitisha Kifungo Chake Cha Gerezani Cha Miaka 7 Na Siku 180 endapo Atakiri shtaka Hilo La Kutumia Silaha Bila Kibali.
Awali Rocky aliwahi kukutwa hana hatia kwa makosa mawili ya jinai kwa madai hayo ya kumpiga risasi #ASAPRelli nje ya hoteli moja mjini Hollywood 2021. Hata hivyo, baada ya kusikilizwa tena shauri hilo kwa takribani siku mbili Nov 2023, Jaji wa Mahakama Kuu alisema kuwa kuna ushahidi wa kutosha wa kumfanya Rocky Kuendelea kusimama kizimbani.
Terrell Ephron maarufu kama A$AP Relli Aliwahi Kukaririwa Akiiambia Mahakama kwamba yeye na A$AP Rocky walikuwa na beef ambalo lilipelekea Rocky kumfyatulia risasi.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.