Ajali Morogoro: Malori yagongana, Watu wawili wafariki Dunia

Watu wawili wamefariki Dunia papo hapo katika tukio la ajali ambayo imehusisha magari mawili baada ya kugongana uso kwa uso katika eneo la Nanenane Manispaa ya Morogoro Barabara Kuu ya Morogoro-Dar es salaam.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkaguzi Faraja Pazzy Mwakilishi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa Saba Usiku wa kuamkia leo Machi 04, 2025 ajali ambayo imehusisha Lori la Mafuta lilokuwa likitokea Dar es salaam likiwa limepakia aina mbili za Mafuta Petrol na Diesel pamoja na Lori la kubeba mizigo lilokuwa likitokea Iringa.

Amesema wamebaini uwepo wa vifo vya watu wawili katika lori hilo la mafuta ambao bado hawajatambulika jinsia na majina yao na kwamba baada ya zoezi la uokozi kukamilika itatolewa taarifa kamili.

#WasafiDigital