Mohammed Iqbal Dar, mtu aliyebuni jina la “Tanzania” amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80 huko Birmingham, Uingereza baada ya kuugua kwa takribani miaka 10.
Mohammed Iqbal Dar, alizaliwa Tanga Agosti 8, 1944 na kupata elimu ya Msingi na Sekondari H.H. The Agakhan na baadaye Mwaka 1964 alijiunga na Shule ya Sekondari Mzumbe, ambapo akiwa Mzumbe aliona Tangazo la Serikali katika Gazeti la The Standard likiwaomba Watu washiriki katika kubuni jina jipya kwa ajili ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Alichukua herufi tatu za kutoka jina la Tanganyika (TAN), herufi tatu za jina la Zanzibar (ZAN), herufi ya kwanza ya jina lake Iqbal (I) na imani herufi ya kwanza ya dhehebu lake la kiislamu la Ahmadiyya (A).
Akaunganisha: TAN+NZAN+I+A akapata jina Tanzania, ambalo linatumika mpaka leo.
Iqbal aliibuka mshindi na kupewa Tsh. 200 na nishani iliyotolewa na Waziri wa Habari wa wakati huo, Sheikh Idrisa Abdul Wakil
Kifo chake ni pigo kwa familia na taifa, lakini jina lake litaishi milele katika historia ya nchi.
Leave a Reply