Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linamshikilia ndugu Lameck Mwamlima mwenye umri wa miaka 29 ambaye ni fundi magari na Mkazi wa Mtaa wa Migombani katika Halmashauri ya Mji Tunduma Wilayani Momba kwa tuhuma za mauaji ya Vicent Mwenda umri (38) ambaye alikuwa katekista wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Yesu lilipo Tazara Tunduma Mkoani Songwe ambaye alivamiwa nyumbani kwake na kisha kushambuliwa na kitu chenye ncha kali.
Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kamanda waPolisi Mkoani Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Mei 20 ambapo tukio la mauaji lilitokea Mei 10 huku chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi na tukio hilo
Limetokea huko Mjini Tunduma.
Leave a Reply