Amorim: United haitakufa, tutakuwa bora tena

Kocha mkuu wa Manchester United, Ruben Amorim (40) ameikingia kifua klabu yake hio baada ya kuwa na maneno mengi nje ya uwanja kuhusu kuporomoka kwa Mashetani wekundu na kuhusishwa hata kushuka daraja.

“Manchester United haiwezi kufa, hilo liko wazi najua mnahisia tofauti mitaani, mashabiki wanapata ugumu wa kulipia tiketi zao na kwenda uwanjani”

“Tunahitaji kuweka nguvu zaidi, kuokoa mustakabali wetu na hatutacheza kama ilivyozoeleka (akimaanisha vibaya)” amesema Amorim 

Manchester United inashikilia nafasi ya kumi na nne (14) kwenye ligi huku wakiwania kombe Moja tu ambalo ni Europa League ambayo wapo katika hatua ya kumi na sita bora.