Ayra Starr Asainiwa Roc Nation Na Jay-Z

Muimbaji Wa Nigeria @ayrastarr Rasmi Amesaini Dili La Usimamizi Wa Kazi Zake Na Label Ya Roc Nation Inayomilikiwa Na #JayZ, Huku Akiendelea Kuwa Chini Ya Mavin Records. Taarifa Hii Ilitolewa Kupitia Akaunti Za Roc Nation, Ambapo Kupitia IG Roc Nation Wamempongeza Ayra Kwa Ushirikiano Wao Huo Mpya.

Hatua hii inatarajiwa kumfungulia msanii huyo milango zaidi ya kimataifa na kuongeza ushawishi wake katika tasnia ya muziki duniani. A

Ushirikiano huu pia unaonyesha jinsi wasanii kutoka Afrika wanavyozidi kutambulika na kupata nafasi kwenye jukwaa la kimataifa.