Balozi wa Tanzania Afrika Kusini awapokea Wanafunzi 28 wa Masomo ya Sayansi, Uhandisi na Sheria

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. James Bwana, leo mchana amewapokea Wanafunzi 16 Watanzania, waliofika nchini humo kwa ajili ya Masomo ya Shahada ya Sayansi katika Masomo ya Kompyuta; Utunzaji wa Taarifa (Data Science) pamoja na Masomo ya Akili Mnemba (Articial Intelligence), kwa Ufadhili wa Mheshiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ujulikanao kama Samia Scholarship Extended.

Wanafunzi wao wamewasili nchini Afrika Kusini kwa Masomo hayo katika Chuo Kikuu cha Johannesburg (UJ).

Mara baada ya Mapokezi katika Uwanja wa Kimataifa wa OR Tambo, Mhe. Balozi Bwana amewasihi Wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwa Mabalozi wazuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini. Aidha, ameipongeza Serikali chini ya Uratibu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi (COSTECH), Ubalozi na Wadau wengine, katika kuratibu upatikanaji wa fursa za masomo ya Shahada nje ya nchi, kwa vijana Watanzania wenye viwango vikubwa vya ufaulu.

Pamoja na Wanafunzi hao 16, hii leo Mhe. Balozi Bwana pia amewapokea Wanafunzi wengine 5 waliofika nchini Afrika Kusini kwa Masomo ya Shahada ya Uhandisi wa Masuala ya Madini, katika Chuo Kikuu cha Johannesburg (UJ), chini ya Ufadhili wa Kampuni kutoka Afrika Kusini inayomiliki Migodi ya Dhahabu nchini Tanzania (Barrick Gold).

Aidha, katika mwendelezo wa kuunga mkono utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023, mwezi Januari 2026 Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini kwa kushirikiana na Shirika la Mastercards Foundation pia uliweza kufanikisha Wanafunzi 7 kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupata Ufadhili wa Masomo nchini Afrika Kusini, kwa Masomo ya Shahada ya Sheria na Uhusiano wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Pretoria (UP).

Mhe. Balozi Bwana ameeleza kuwa jitihada za Ubalozi kuunga mkono utekelezaji wa Vitendo wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, Toleo la 2023 ni endelevu na Ubalozi utaendelea kutafuta fursa zaidi ili kutekeleza kwa vitendo dhamira ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kujenga taifa imara la vijana wa kitanzania walioandaliwa vema kukidhi mahitaji ya kidigitali ya karne hii, na hivyo kuwa na mchango zaidi kwa maendeleo ya Taifa.