Mahakama ya Mkoa wa Bioko nchini Guinea ya Ikweta imemhukumu Baltasar Engonga, aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha (NFIA), kifungo cha miaka nane (8) jela kwa makosa ya ubadhirifu wa fedha za umma na kujitajirisha kinyume cha sheria.
Engonga amehukumiwa pamoja na maafisa wengine watano waandamizi, ikiwemo Mangue Monsuy Afana, Baltasar Ebang Engonga Alú, na Rubén Félix Osá Nzang, baada ya kupatikana na hatia ya kufuja pesa za umma. Mahakama pia imewaamuru walipe mamilioni ya dola kama faini.
Engonga aligonga vichwa vya habari duniani kote mwaka 2024 baada ya kusambaa kwa kasi kwa video za ngono zaidi ya 400 zilizopatikana kwenye vifaa vyake vya kielektroniki, ikiwemo kompyuta yake mpakato, wakati wa uchunguzi wa makosa ya ufisadi.
Leave a Reply