Bashungwa ipa agizo NIDA, Vitambulisho 31,000 Vyakutwa na Changamoto

Serikali kupitia kwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Innocent Bashungwa, imeiagiza Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuvirejesha kutoka kwa Wananchi takribani Vitambulisho vipatavyo 31,000 vilivyokutwa na Changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya Kufutika kwa maandishi, huku akieleza kuwa tayari Changamoto iliyosababisha hali hiyo imetatuliwa.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo Jijini Dar es Salaam leo Januari 13, 2025 wakati wa kikao kazi chake na Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) ikiwa ni mara yake ya kwanza kuketi nao mara baada ya Kuteuliwa Kushika wadhifa huo na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

“Kutokana na hilo nimetoa maelekezo kwa NIDA, wahakikishe wanavirejesha Vitambulisho hivyo kutoka kwa Wananchi haraka, na Vichapishwe vingine kwa ajili ya wananchi hao 31,000 na Wasitozwe Chochote kutokana na Zoezi hilo” amesema Waziri Bashungwa.