Kwa mujibu wa TMZ, rapa Busta Rhymes, mwenye umri wa miaka 52, anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya shambulio kufuatia tukio la ugomvi na msaidizi wake, kwa mujibu wa vyanzo vya utekelezaji wa sheria. Tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita asubuhi huko Brooklyn, ambapo mzozo wa maneno kati ya rapa huyo na msaidizi wake mwenye umri wa miaka 50 ulizidi na kuwa ugomvi Uliopelekea Wawili Hao Kushambuliana. Busta anadaiwa kumpiga ngumi msaidizi wake usoni kabla ya kuondoka eneo la tukio.
–
Msaidizi huyo aliita polisi kwa Kupiga simu ya dharura (911), na maafisa wa usalama walimpeleka hospitalini Kwa Ajili Ya matibabu. Busta Rhymes baadaye alijisalimisha kwa polisi Jumanne na kutakiwa kufika mahakamani. Sasa anakabiliwa na mashtaka ya shambulio la daraja la tatu (third-degree misdemeanor assault), jaribio la shambulio, na unyanyasaji.
Jaribio la kuwasiliana na wawakilishi wa rapa huyo kwa maoni halijafanikiwa mpaka sasa.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.