Cardi B Anatuhumiwa kwa Unyanyasaji Wa Kiuchumi

Baada ya miaka kadhaa ya kuharibu sifa ya rapa Cardi B kupitia video za YouTube na machapisho ya mtandaoni, mwanaharakati wa mtandao Tasha K ambaye alitakiwa kumlipa Cardi B, sasa anajaribu kubadili mwelekeo wa madai hayo.

nyaraka mpya za mahakama zilizopatikana na TMZ, Tasha K anadai kuwa Cardi B anamnyanyasa kiuchumi kwa kudai kuwa ameweka wazi akaunti zake za siri zilizoko kwenye visiwa vya Cook, Nevis, na Georgia.

Zaidi ya hayo, Tasha K anadai kwamba Cardi B amekuwa akijaribu kuhujumu kesi kwa kutaka masharti ya makubaliano ya kulipa deni yaweze kumzuia kuzungumzia chochote kumhusu rapa huyo kwenye blogu na mitandao ya kijamil.

Haya yanajiri miaka mitatu baada ya mahakama kumuamuru Tasha K kulipa fidia ya zaidi ya dola milioni 3.4 kwa kumkashifu Cardi B kama kahaba mtumiaji wa dawa za kulevya mwenye magonjwa ya zinaa.