Rapa Cardi B Hivi Karibuni Kwenye Mahojiano Na @billboard Amewachana Wasanii Wanaozikosoa Tuzo Za Grammys Huku Wakiwasilisha Kazi Zao Kwa Siri. Cardi Alizungumza Hayo Na Billboard Ikiwa Yupo Mbioni Kuachia Album Yake Mpya ‘Am I The Drama?’.
“Nikiwasilisha Album Yangu Au Kazi Zangu… Ikitokea Nimekosa Basi Basi Nimekosa…. Inabaki Kuwa Hivyo, Huo Ndio Uhalisia. Lakini Kamwe Sitokuja Kuzichukia…… Sitokuja Kuwa Kama Wale Wanaosema …(Oooh Hizo Tuzo Ni Za Mchongo, Hazina Maana Yoyote) Hapana …Hizo Tuzo Zinamaana Na Ndio Maana Wote Mnazifukuzia … Acheni Masihara”
Utakumbuka 2019 Cardi B Alishinda Tuzo Ya Grammy Ya ‘Best Rap Album’ Kwa Album Yake Ya Kwanza Iitwayo ‘Invasion Of Privacy”. Unaambiwa Ushindi Huo Aliupata Akiwa Katika Kipindi Kigumu…..Alikuwa Mjamzito, Anaumwa, Kubadili Sana Managers Pamoja Na Kushughulia Kesi Za Mahakamani Wakati Akiwa Anaendelea Kufanyia Kazi Ngoma Mpya.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.