Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kimesema, viongozi, wanachama na waandishi wa habari ambao jumla yao ikiwa ni ishirini na tano ndio waliokamatwa na Jeshi la polisi April 24 mwaka huu katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam na kwamba idadi iliyotajwa na jeshi hilo ni ndogo kulingana na ripoti yao.
Hayo yamebainishwa leo Aprili 30, 2025 na Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho Mikocheni Jijini Dar es Salaam, na kuyataja madhira mengine yaliyojitokeza kwa waliokamatwa.
Aidha, Kupitia kwa Katibu mkuu huyo CHADEMA imetoa matamko kuelekea kwa mamlaka za uteuzi, Ofisi ya Rais, Jeshi la polisi Tanzania na kwamba inadhamiria kuchukua hatua kadhaa za kisheria ngazi za kimataifa.
Leave a Reply