Mkuu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jenerali Jocob John Mkunda ametangaza nafasi za kuandikishwa Jeshi la wananchi Kwa vijana wenye elimu ya Sekondari hadi elimu ya Juu.
Akizungumza leo aprili 30,2025 Makao ya Jeshi Hilo msalato Jijini Dodoma Kwa Niaba ya Mkuu huyo wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania Msemaji wa Jeshi hilo Kanali Gaudentius Ilonda amesema kuwa nafasi zinazoandikishwa na Jeshi hilo ni kwa vijana wenye elimu ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita umri usiozidi miaka 24, Vijana wenye elimu ya Stashahada umri usiozidi miaka 26, Vijana wenye elimu ya Juu umri usiozidi miaka 27 na Madaktari Bingwa wa
Binadamu umri usiozidi miaka 35 ya kuzaliwa.
Kanali Ilonda amesema kuwa utaratibu wa Maombi hayo yaandikwe Kwa mkono na Muda wa kuwasilishwa Maombi hayo ni kesho mai 1 ,2025 na mwisho mai 14 2025 na yaambatanishwe na nakala ya kitambulisho Cha Taifa pamoja na namba ya NIDA, nakala ya cheti Cha kuzaliwa, Cheti Cha shule, chuo na namba ya simu ambayo itakuwa rahisi Kwa mawasialiano.
Aidha Kanali Ilonda ametoa angalizo baada ya kutangaza nafasi hiyo ya kuandikishwa Jeshini ambapo amesema kuwa wananchi wasikubali kutapeliwa na matapeli Kwa kisingizio Cha kupata nafasi ya Jeshi Kwa kutoa fedha
“Nitoe angalizo Kwa wananchi Hakuna nafasi ya kuandikishwa Jeshini Kwa kutoa fedha msikubali kutapeliwa” – amesema Kanali Gaudentius Ilonda
Fred christopher kaleza
S.L.P 05,
Kwaalinatoo-zanzibar
0675679105
Makao makuu dodoma
Mkuu wa utumishi jeshini
S.L.P 2963
Dodoma
Yah: MAOMBI YA KUJIUNGA NA JESHI LA ULINZI TANZANIA (JWTZ).
husika na kichwa cha habari hapo juu.
Mimi ni kijana Mtanzania, mwenye umri wa miaka 21, mwenye namba ya utambulisho wa nida , 20040307-7110800001-24, nimehitimu masomo yangu ya elimu ya sekondari mwaka 2022, shule ya sekondari st.paul kiungani zanzibar, kwa mujibu wa tangazo lenu lililotolewa na jeshi la ulinzi tanzania, ninaomba nafasi ya kujiunga na jeshi la ulinzi wa Tanzania JWTZ.
Pamoja na barua nimeambatanisha vivuli vya vyeti vangu kama tangazo lilivyoagizwa,
Natumai ombi langu litapokelewa.