CHADEMA Zanzibar wataka mabadiliko kuelekea uchaguzi mkuu 2025

Kamati Maalum ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA upande wa Zanzibar imesema miongoni mwa maazimio ya kamati hiyo ni pamoja na hoja ya kutokuwa tayari kuingia kwenye uchaguzi bila ya kufanyika kwa yale waliyoita mabadiliko ya kisheria

Taarifa ya maazimio ya kikao hicho imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari Uenezi na Mawasiliano kwa Umma CHADEMA Zanzibar Hamad Mussa Yussuf wakati akizungumza na waandishi wa habari siku chache baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Maalum ya Chama hicho Zanzibar kilichoketiwa Mei 28, mwaka huu

Mussa amesema chama hicho kimeelekeza kuwepo kwa mabadiliko ya sheria ikiwemo kutungwa kwa sheria mpya ya uchaguzi, kuondosha uchaguzi wa siku mbili pamoja na kuwekwa uwiano wa kura wakati wa kuchagua viti maalum katika baraza la Wawakilishi na sio uwiano wa viti vya wajumbe wa baraza hilo kama ilivyo sasa