Chelsea mbabe wa makombe ya UEFA

Klabu ya Chelsea imeweka rekodi ya kipekee barani Ulaya kwa kuwa klabu pekee katika historia ya soka la Ulaya kushinda mataji yote makuu manne ya UEFA.

Hadi sasa, Chelsea ndio timu ya kwanza na ya pekee kufanikisha ushindi katika mashindano haya yote:
UEFA Champions League
Chelsea walitwaa taji hili kubwa ulaya kwa mara ya kwanza mwaka 2012, baada ya kuwashinda Bayern Munich kwa mikwaju ya penati. Walirudia mafanikio hayo mwaka 2021, walipoifunga Manchester City bao 1-0 katika fainali iliyochezwa jijini Porto, Ureno.
UEFA Europa League
The Blues walitwaa taji hili mwaka 2013 chini ya kocha Rafael Benítez, na kisha wakalishinda tena mwaka 2019 chini ya Maurizio Sarri, baada ya kuichapa Arsenal mabao 4-1 katika fainali iliyofanyika Baku, Azerbaijan.
UEFA Super Cup
Chelsea walifanikiwa kutwaa taji hili la wakikipiga kati ya mabingwa wa Champions League na Europa League mwaka 2021, walipoifunga Villarreal kwa mikwaju ya penati baada ya sare ya bao 1-1.
UEFA Europa Conference League
Hili ni taji jipya lililoanzishwa na UEFA mwaka 2021. Chelsea walikamilisha safu ya ushindi wa mataji yote makuu kwa kulinyakua taji hili hapo jana Mei 28, 2025 kwa kumchapa Real Betis kichapo cha mabao 4-1.

Kwa mafanikio haya, Chelsea sasa wamejiweka katika nafasi ya kipekee kabisa katika historia ya vilabu vya Ulaya. Hakuna klabu nyingine – hata zile zenye mafanikio makubwa kama Real Madrid, Bayern Munich au AC Milan – iliyowahi kushinda mataji haya yote manne.