Msanii wa Muziki wa kizazi Kipya Rashidi Makwiro Chid Benz, amesema anawajua wasanii wanaotumia dawa za kulevya hivyo kawashauri kujitoleza kabla hawajatajwa ili wapate kusaidiwa na serikali kupata tiba ya kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya na kuwashauri wasiojihusisha na dawa za kulevya kuepuka kwani mwisho wake sio mzuri.
Chid Benz ameyasema hayo mbele ya kamishina jenerali wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Aretas Lyimo na katibu mtendaji wa baraza la sanaa Basata Dkt Kedmon Mapama, mara baada ya kutoka soba alikokuwa akipatiwa matibabu kwa kipindi cha miezi sita.
Hata hivyo Chidbenz amesema kuwa anaishikuru serikali kupitia DCEA, Basata pamoja na watanzania wote waliokuwa wakimuombea kwa kipindi chote alichokuwa akipatiwa matibabu, na kuongeza kuwa kwa matibabu aliyoyapata hivi karibuni hawezi Kurudia matumizi ya dawa za kulevya na yupo tayari kuendelea na kazi zake za Mziki.
Leave a Reply